Hii ya Wizkid kuwapiga ‘vikumbo’ Jay Z na Drake nayo ni kubwa ya Afrika (+video)

Mastaa wa Muziki kutoka Nigeria, Wizkid na Davido wamezibeba headlines za MOBO AWARDS 2017 ambapo Wizkid amevunja rekodi kwa kuwa msanii pekee kutokea Afrika kushinda tuzo ya Msanii bora wa kimataifa katika tuzo hizo zilizotolewa Uingereza.

Kwenye kipengele alichokua anawania Wizkid, alikua akipambanishwa na Wakali wa kimataifa kama Cardi B, DJ Khaled, Drake, Jay Z, Kendrick Lamar, Migos, Solange Knowles, SZA, Travis Scott ambapo hii sio mara ya kwanza Wizkid kupata ushindi MOBO AWARDS, aliwahi pia kushinda mwaka 2011 na 2016.

Davido pia ameshinda tuzo kama Msanii bora wa Afrika ambapo alikua anachuana na Eugy, Juls, Maleek Berry , Mr Eazi, Sarkodie, Tekno, Tiwa Savage na Wande Coal.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*