MAMA WEMA YAMKUTA MAZITO BAADA YA MWANAE KUTOFIKA MAHAKAMANI NA HAKIMU KUAMUA HILI…..

MAMA wa Miss Tanzania 2006 na msanii wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu, Miriam Sepetu, leo alionywa na hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba baada ya mwanae huyo kushindwa kufika mahakamani ambapo anakabiliwa na kesi la matumizi ya madawa ya kulevya.

Katika kesi hiyo Wakili wa Serikali Agustino Michael aliitaja kesi hiyo mbele ya hakimu Simba kuwa ndiyo iliyokuwa ikitakiwa kuendelea lakini mama Wema alinyoosha kidole kuashiria kuwa na neno.

Hakimu huyo alimkaribisha mama Wema kusema jambo alilotaka kusema ndipo akaanza kutoa hudhuru na kuiambia mahakama hiyo kuwa Wema alishindwa kufika mahakamani hapo kufuatia kufiwa na shangazi yake.

“Mheshimiwa Wema amefiwa na shangazi yake hivyo ameenda kushughulikia suala la mazishi ndiyo maana hakuweza kufika hapa mahakamani mimi ndiyo nimekuja kumuwakilisha” alisema Mama Wema.

Baada ya mama huyo kutoa hudhuru huo hakimu alianza kumbana maswali ambapo alimuuliza kama Wema amepatwa na msiba uliomfanya ashindwe kufika mahakamani imekuwaje yeye mama yake apate muda huo yeye ashindwe?

Aliuliza hakimu huyo kisha kumuonya mama Wema kwa kumuambia siku nyingine asichukulie masihara suala la mshitakiwa huyo kuripoti mahakamani.
Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Desemba 14 mwaka huu.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*