DAAH MAAJABU MWANAUME AKAMATWA KUKUTWA NA SEHEMU NYETI ZA MWANAMKE NA KUDAI KUWA NI…..

Salum Nkonja akiwa chini ya ulinzi wakati akipelekwa mahakamani leo.

…Akishuka ngazi baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabili kupelekwa rumande.

SALUM NKONJA (22) mkazi wa Ipililo wilayani Maswa mkoani Shinyanga leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na tuhuma za kumuua mtu asiyejulikana.
Tetesi za kesi hiyo zinasema kijana huyo alikamatiwa katika kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam akiwa na viungo vya binadamu ambavyo ni sehemu za mbalimbali za siri za mwanamke na nyara za serikali.
Nkonja ambaye amesomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha, hakutakiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
Wakili wa serikali, Nassoro Katuga, akisoma hati ya mashtaka, amedai kati ya Oktoba Mosi na 30 mwaka huu katika eneo la Kahama mkoani Shinyanga na kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam, alimuua mtu ambaye bado hajafahamika.
Kesi imeahirishwa hadi Decemba 8, mwaka huu kwa vile upelelezi bado haujakamilika na mtuhumiwa amepelekwa rumande.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*