OKWI ATOA MANENO HAYA KWA WANA WAMSIMBAZI BAADA YA ……

Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi amesema atarejea kwa kasi na uwezo zaidi baada ya kuwa nje kwa muda akiuguza majeraha aliyoyapata akiwa kwenye majukumu na timu ya taifa ya Uganda.

Okwi ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram akielezea namna ambavyo ameukumbuka mchezo wa mpira wa miguu kutokana na kutocheza kwasababu ya kuwa majeruhi.
“Hakika nimeukumbuka sana mpira wa miguu, lakini nitarejea nikiwa imara zaidi baada ya kupona majeraha madogo yanayoniweka nje ya uwanja” ameandika Okwi”.

Okwi ambaye ni kinara wa mabao kwenye ligi kuu soka Tanzania bara akiwa na mabao 8 aliumia kwenye kambi ya The Cranes ilipokuwa ikijiandaa na mechi ya kukamilisha ratiba ya makundi kuwania kufuzu kombe la dunia dhidi ya Ghana.
Klabu ya Simba inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na alama ya 22, ikifuatiwa na klabu ya Azam FC yenye alama 22, huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na mabingwa watetezi Yanga SC yenye alama 20.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*