CHANZO KIFO CHA MUME WA UWOYA NDIKUMA CHABAINIKA UKWELI MTUPU HUU HAPA….

Asubuhi ya leo Tanzania imezipokea taarifa za kifo cha aliyekuwa Kocha msaidizi wa timu ya Rayon Sports ya Rwanda, Hamad Ndikumana Katauti ambae amefariki ghafla.

Mwandishi wa habari za Michezo Shaffih Dauda ameripoti kwamba Gakwaya Olivier ambae ni Afisa Habari wa Timu hiyo amesema Ndikumana amefariki kwa kile kinachosadikiwa kuwa ni ugonjwa wa moyo.

“Alisikia maumivu makali kifuani akaomba soda ya baridi wakamletea na alipomaliza kunywa tu kidogo akatapika na akaishiwa pumzi na ndipo akakata kauli, bado tunasubiri uchunguzi wa kina wa kitabibu”

Marehemu aliwahi kucheza soka Tanzania akiwa na Stand United na ni Mume wa zamani wa Mwigizaji Irene Uwoya na wana mtoto mmoja. RIP Ndikumana

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*