Waandamana kupinga ibada ya Waislamu barabarani Paris

Takriban wanasiasa 100 wa Ufaransa wameandamana katika barabara za makaazi ya Paris kupinga hatua ya Waislamu kufanya ibada ya maombi hadharani.

Wanasiasa hao waliokuwa wakiimba nyimbo ya taifa hilo waliwaondoa takriban wafuasi 200 wa dini ya Kiislamu waliokuwa wakiomba barabarani katika eneo la Clichy.

Maafisa wa polisi hatahivyo walifanikiwa kuyatawanya makundi hayo mawili, Wakosoaji wanasema ni makosa kwa wafuasa hao wa dini kutumia eneo la umma ambalo linatumika na watu wa dini tofauti.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*