Sitti awaomba Watanzania kujitokeza kwenye fursa za ajira

Watanzania wameombwa kujitokeza katika usaili ulioanza kufanyika katika maeneo ya National Housing karibu na uwanja wa taifa ili kupata watu wenye fani na sifa mbalimbali.

Kupitia kampuni ya Bravo Job Centre Agency Limited ya malkia wa urembo nchini Tanzania, Sitti Mtemvu imeendesha zoezi la kufanya usahali kwa vijana wanaohitaji kazi ya udereva huku akiongeza siku moja zaidi ya kufanyika zoezi hilo kutokana na muamko mkubwa wa Watanzania.

“Tunaishukuru Kampuni kubwa ya Almarai ya Saudi Arabia kwa kutupa nafasi za kazi watanzania, hii ni fursa nzuri ambayo imekuja kupitia kampuni yetu na kama ambavyo leo umeona jinsi watanzania walivyojitokeza kwa wingi na kuchangamkia fursa, sisi tumeona siku moja haitoshi tumeongeza siku moja ambapo kesho hili zoezi litaendelea ili watanzania wapate nafasi kwasababu bado tuna nafasi nyingi zaidi,”

Sitti amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika usahili kwani nafasi ni nyingi na wanachotakiwa kuwa nacho ni leseni, passport ya kusafiria pamoja na kujua kingereza za mawasiliano.

Pia alisema nafasi nyingine za ajira ambazo watazitoa kwa siku ya kesho ni pamoja na udereva, wauzaji, wapishi wa mahoteli ambapo amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kwani nafasi ni nyingi.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*