Morocco yafuzu kombe la Dunia, Ivory Coast yatupwa nje

TIMU ya taifa ya Morocco imekata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Urusi baada ya kuwapiga wenyeji, Ivory Coast mabao 2-0 mjini Abidjan.

Simba wa Atlas waliingia kwenye mechi hiyo Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny wakiwa wanawazidi pointi moja Tembo wa Ivory Coast na walihitaji sare tu ili kupata nafasi ya kwenda Urusi mwakani.

Hata hivyo, mabao mawili ndani ya dakika tano kutoka kwa Nabil Dirar na Medhi Benatia yaliwapa ushindo mzuri katika mechi hiyo ya Kundi C.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*