POVU LAMTOKA NEY WA MITEGO BAADA YA NGOMA YA HALLELUJAH YA MKALI DIAMOND….

Msanii wa muziki Bongo, Nay wa Mitego amefunguka juu ya wasanii wanaotumia uchawi katika muziki wao.

Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Makuzi’ ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa msanii akiamini katika ushirikina kuna kipindi kile anachokiamini kinaishiwa nguvu.

“Umefika muda karibia Tanzania nzima inaamini kwenye kile ambacho nakifanya, hii ni ndele tosha, ni zaidi ya ndele, sijua mtu ambaye anaamini hivyo” amesema Nay.

“Halafu ndele huwa zina mwisho ukifika muda maana wewe ndio umemaliza hata uimbe vipi, hata umshirikishe yesu bado watu hawaelewi” ameongeza.

Katika hatua nyingine Nay amezungumzia uwezo wake katika performance jukwaani kwa kudai kuwa yeye Juma Nature wa pili kwani msanii huyo amekaa muda mrefu bila kutoa nyimbo ila bado anakubalika.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*