MAPENZI….MBINU7 ZA KUCHAGUA MWENZA AMBAYE HATAKUACHA…

NIMETAMBUA kuwa wakati wa kuchagua mwen­za, watu wengi hupungukiwa na ufunguo wa kuamua kuwa siku moja nitapata mwenza ambaye hataniacha.
Kwanza watu wengi hushindwa kuuliza maswali yanayohusiana na historia aliyokuwa nayo huyo mwenza kabla ya kukutana naye. Ni kosa kubwa sana. Jambo la pili wanadharau tabia zinazojitokeza mwanzoni. Kwa kufikiria kuwa watamwogopesha mwenza ambaye anataka kuwa naye.
Wengine husema kuwa hata kama kulikuwa na tatizo sihitaji kulifahamu. Lakini leo nitakupa mbinu kadhaa za kukusaidia kumchagua mtu na kujitoa kwake.

MWENYE MAHUSIANO MAZURI ALIKOTOKEA
Kutokana na historia yake ya huko nyuma itakuwa ndiyo dalili ya kuonyesha kuwa huyo mtu ana mahusiano mazuri. Kwa mfano huyo mtu kama anaishi vizuri na jamii yake, familia yake, wazazi wake, marafiki zake. Unaweza kujitoa kwake kwa sababu ni mtu mzuri, ana nguvu ya kutunza mahusiano.
AWE MWENYE MFANO WA KUIGWA

Chagua mtu ambaye ana uelewa, hata kama ametoka kwenye familia ambayo wazazi wake waliachana, lakini ni vizuri kujua kama ameathirika vipi kutokana na hali hiyo ya kutengana kwa wazazi wake.
Wengine hupata funzo kubwa la kutatua matatizo yanapotokea kwa sababu ya kuwa na uzoefu huo. Na atakuletea matokeo mazuri. Lakini mwingine anaweza akawa ameathiriwa kabisa na matatizo hayo.
ANAYEWEZA KUYAKABILI MATATIZO

Mtu mwenye uwezo wa kukabiliana na shida mbalimbali huyo ni wa kushikana naye. Huu ni uelewa wa tofauti tena ni
muhimu kujitolea, kuwa mkweli na mtu mwenye kupenda umoja.
Watu wenye hofu mara nyingi huogopa kukutana na matatizo yanapotokea. Ni rahisi kukimbia.
MWENYE HURUMA

Mtu anayeweza kukuelewa maumivu yako na kukufanya ujisikie vizuri, ni mtu ambaye hataweza kukuacha unapokuwa unapitia aina yoyote ya tatizo. Chukua mtu mwema na mwenye huruma, mtu mwenye moyo, na ambaye haogopi kufungua moyo wake kwako.
MWENYE MAWASILIANO MAZURI
Niamini mimi. Ni vizuri kuwa na mtu anayeweza kuongea kuliko yule anayemeza maneno. Yule anayetambua umuhimu wa kuwasiliana kuliko yule anayetegemea mawasiliano.
ANAYEPENDA KUWA KARIBU

Chagua mtu anayependa kuwa karibu yako, anayependa kukugusa, mtu ambaye anakukumbatia kwa mikono yake kwa muda wa kutosha.
Ambaye anapenda kukushika mikono yako, mtu ambaye anapenda kukubusu. Kugusana inafanya kitu kizuri kwenye mahusiano. Chagua mtu anayekufurahia uwepo
wako, anayefurahia kuongea na wewe.
Unapokuwa na mtu huyo hujisikii kuwa peke yako.
MNAYEENDANA KIFIKRA

Ni vyema ukampata mtu ambaye mnaendana kifikra. Au hata kama hamuendani lakini mna moyo wa kusapotiana.
Kama wewe ni mchezaji wa mpira, tafuta mcheza mpira. Kama unaimba tafuta muimbaji au anayependa unachokifanya.
Nakumbuka mama mmoja, wakati ambao aliolewa, mume wake hakuwa mchungaji, lakini kumbe ndani ya huyo mume kulikuwepo roho ya kichungaji.
Ilipojitokeza, mama huyo alikataa kuwa mama mchungaji. Alichofanya ni kuamua kuondoka. Kwa hiyo tafuta mtu ambaye atapenda kitu unachokifanya. Itakusaidia sana.
Wapendanao wanapaswa kuimba ‘wimbo’ mmoja katika safari yao. Kusiwepo na mabishano ndani, mwanamke amsikilize mwanaume, mwanaume naye amsikilize mwanamke pale inapostahili.
Tumieni lugha rafiki kushauriana, kukosoana, kufundishana. Mkiishi kwa kusikilizana, kupendana, uhusiano wenu utastawi hadi wenyewe mtashangaa.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*