KIMENUKA BUNGENI VITA YA ZITO NA SPIKA YAFIKA PATAMU MAMBO MAZITO YAIBUKA SHUHUDIA TIMBWILI HILI….

Spika wa Bunge, Job Ndugai.
MBUNGE wa Kigoma Mjini (ACT –Wazalendo), Zitto Kabwe amekamatwa na polisi akiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) akitokea Kigoma.
Ofisa Habari wa ACT-Wazalendo, Abdallah Khamis amesema Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa chama hicho amekamatwa jana jioni.

Jana, Jumatano asubuhi, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alisema Zitto atafutwe, akamatwe na kufikishwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.
Alisema Zitto alipewa barua ya wito wa kufika mbele ya kamati hiyo baada ya Spika Job Ndugai kuagiza hilo lifanyike lakini hajalitekeleza.
UDATES

Taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya ACT-Wazalendo, Mohamed Babu imesema Zitto amesafirishwa kwa gari saa 10:00 usiku akitokea kituo cha polisi cha Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA).
Amesema kamati hiyo inafuatilia kwa umakini hatua kwa hatua kuhakikisha usalama wake ikiwataka wanachama na wananchi kuendelea kuwa watulivu.

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu amesema Zitto amesafirishwa kwa gari la Bunge akiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Zitto anatakiwa kufikishwa mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*