TANZIA…YANGA YAPATA PIGO ZITO MZEE LWANDAMINA AFARIKI DUNIA HIVI PUNDE…

Klabu ya Yanga yapatwa na msiba wa kuondokewa na baba yake mzazi kocha mkuu mwenye uraia wa Zambia, George Lwandamina.

Hayo yamethibitishwa na Afisa habari wa klabu hiyo Dismas Ten na kusema ni kweli kocha wao amepatwa na msiba wa mzazi wake huko kwao Zambia na tayari wameshafanya mpango wa kumsafirisha Lwandamina kwenda kuhudhuria msiba huo.
“Lwandamina ameondoka leo nchini Tanzania kuelekea nyumbani kwao Zambia kwa ajili ya mazishi ya baba yake, ila akifika huko ndiyo tutaweza kujua tarataibu za mazishi kwa kuwa shuguli zote zinafanyikia huko kwao”, alisema Ten.

kocha mkuu wa Yanga George Lwandamina
Lwandamina ambaye amejiunga na Yanga Novemba, mwaka jana (2016) inadaiwa baba yake mzazi alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kupooza na kufariki usiku wa Jumanne Agosti 29 mwaka huu.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*