JUX ALIZWA NA PENZI LA VANNESA MDEE HATIMAE AKUBALI KUSEMA SIRI NZITO YA PENZI LAO…

Msanii wa muziki bongo fleva Juma Jux aonyesha bado anahitaji uwepo wa aliyekuwa mpenzi wake msanii Vanessa Mdee, kwa kushindwa kuvumilia maumivu ya kuachana na kuweka bayana kwamba atafarijika sana endapo atamuona tena kwa mara nyingine.

Jux amebainisha hayo kupitia ukurasa wake Instagram ambapo ameandika ujumbe unaohusu kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, na kusema miaka ya nyuma alikuwa hafanyi sherehe kutokana alikuwa na mpenzi wake Vanessa kwenye siku hiyo nakujiona kama amesherehekea lakini kwa sasa hayuko naye tena anatamani hata aende kuhudhuria tu kama rafiki na itakuwa faraja kubwa kwake.

” Sikuwahi kufanya ‘party’ yoyote tena sababu nilikuwa na rafiki, mpenzi na mtu wa karibu kuliko mtu yoyote kwenye maisha yangu. Sasa hatuko tena karibu kama mwanzo, tumebaki kuwa marafiki wa kawaida tu. Uwepo wake tu ulikuwa ni zaidi ya chochote kwenye siku yangu ya kuzaliwa, kuongea na yeye au ujumbe wake tu ilitosha kukamilisha siku yangu. Ila sasa sidhani kama itakuwa kama mwanzo, nitafarijika sana kama nitamuona hiyo siku”, aliandika Jux.

Jux hivi karibuni akiwa kwenye mahojiano na kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, amekiri kuwa bado ana hisia juu ya Vanessa Mdee, ambaye pia alishawahi kusikika akikiri bado anampenda Jux na ataendelea kumpenda.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*