Hivi Ndivyo Dkt. Cheni Alivyonusurika Kifo Baada ya Kupata Ajari Mbaya….

Muigizaji wa kitambo Bongo, Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’ amenusa kifo baada ya kupata ajali mbaya baada ya gari lake kupasuka tairi la mbele na kuparamia nguzo kisha kupata maumivu makali kwenye bega la mkono wa kushoto.

Kwa mujibu wa shuhuda wetu, Cheni alikumbwa na mkasa huo usiku wa Alhamisi iliyopita maeneo ya Bamaga-Mwenge, Dar, wakati akitokea Tegeta kwenye sherehe ya mmoja wa jamaa zake ambapo alipofika eneo hilo, ghafla tairi la upande wa kulia lilipasuka na kukosa mwelekeo kisha kuivaa nguzo iliyopo pembeni kabla ya kukwama kwenye jiwe kubwa.

“Dah! Ni kweli nilipofika pale Bamaga, ghafla nilisikia gari limekuwa zito na hapohapo tairi la mbele likapasuka. Gari lilikosa mwelekeo nikalielekeza kwenye nguzo, ninamshukuru Mungu sikupata jeraha kubwa, nimeumia bega la kushoto ila ninaendelea vizuri,” alisema Dk Cheni.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*