HABARI ZA HIVI PUNDE….ASKOFU GWAJIMA YAMKUTA MAZITO NDIO BASI TENA…..

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo July 31, 2017 imekwama kutoa hukumu ya kesi ya kushindwa kuhifadhi silaha inayomkabili Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kwa sababu anaumwa.

Akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa ambapo Wakili wa Serikali, Shadrack Kimaro alieleza shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutolewa hukumu ambapo hata hivyo, Wakili wa utetezi, Peter Kibatala amedai kuwa mteja wake ameshindwa kufika Mahakamani kwa sababu anaumwa.

Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi August 30, 2017 kwa ajili ya hukumu.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*