MICHEZO…..B Dozen, Mamy Baby, DJ Cynyorita, DJ Zero wakiishuhudia chama lao Keko Furniture Ndondo Cup…

Jumapili ya July 30 2017 chama la wana Keko Furniture linalosapotiwa na team XXL lilicheza mchezo wa robo fainali ya mwisho dhidi ya Stimtosha ambao ni team Alasiri, Team XXL ambao waliongozwa na brand meneja wao B Dozen wote walikupo Kinesi kuangalia game.

Jukwaa Kuu Mkurugenzi wa uzalishaji na utafiti Clouds Media Group Ruge Mutahaba alikuwepo kufuatilia mchezo

Keko Furniture leo wamefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano ya Ndondo Cup 2017 kwa ushindi wa mikwaju ya penati 4-3 hiyo ni baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika kwa sare ya kufunga goli 1-1, game hiyo ilishuhudiwa na team nzima ya XXL ambao wanaisapoti.

Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete alikuja kuisapoti Stimtosha ambayo imetolewa

Ushindi wa Keko unaipeleka nusu fainali na sasa watasubiri hadi kesho jioni kujua watacheza na timu gani katika hatua ya nusu fainali baada ya droo itakayochezeshwa LIVE, timu zilizofuzu kucheza hatua ya nusu fainali ni Kibada One, Misosi FC, Goms United na Keko Furniture waliyofuzu leo.

Mameneja wa WCB Babu Tale, Mkubwa Fella na Makame

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*