BREAKING NEWS: WATANGAZAJI WA REDIO NA TV HII KUBWA NCHINI WAPATA AJALI YA NDEGE HIVI PUNDE…

Watangazaji wa Radio Citizen na Citizen TV za nchini Kenya, wamenusurika kufa baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuelekea Karbanet, kupata ajali katika eneo la Kibra jijini Nairobi.

Taarifa kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa Ndege za Polisi, Rodgers Mbithi zinaeleza kwamba ndege hiyo ilianguka muda mfupi baada ya kuruka kutoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Wilson, ikiwa na wanahabari watatu waliokuwa wakielekea kwenye mkutano wa NASA, ndipo ajali hiyo ilipotokea.

Ndege hiyo, CESNA 206 ilikuwa imewabeba watangazaji wa Citizen TV ambao ni; Sam Ogina, Cameraman Mauritius Oduor na Joseph Njane wa Radio Citizen.

Majeruhi wote wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*