MAPENZI: JINSI YA KUJIWEKA WA THAMANI KWA MPENZI WAKO….

Marafiki zangu tunaendelea na mada yetu ambayo kwa hakika imekuwa ndefu lakini yenye manufaa makubwa kwenye uhusiano wetu. Nilianza kwa kueleza kwamba yapo mambo mengi sana ambayo husababisha thamani ya mtu kushuka kwa mpenzi wake.

Nilishazungumza mengi katika matoleo yaliyopita lakini leo nitaendelea na kukazia zaidi kwenye athari za kuharakisha faragha. Karibu darasani.

ATHARI ZA KUHARAKISHA FARAGHA
Wiki iliyopita nilifafanua zaidi matatizo ya moja kwa moja ambayo mtu anaweza kuyapata kwa kuharakisha faragha ambapo nilisema kwamba kuna suala la kuchokwa na kuonekana wa kawaida.

Lingine ni kuonekana mwepesi kwenye suala la mapenzi hivyo mwanaume kuwa na mashaka kwamba hata kama akifikia uamuzi wa kukuoa unaweza kuwa mwepesi kutoa penzi kwa wengine kama ulivyofanya kwake. Tuangalie vipengele vinavyofuata.

(i) Hupunguza thamani
Heshima ya penzi ni kwenye ndoa. Kuna uwezekano mkubwa sana wa kushushwa thamani baada ya kutoa penzi. Wanaume wengi huanza kuwa wasumbufu (kama ni kasumba yao) kwa wapenzi wao baada ya kutoka nao kimapenzi.

Pamoja na kwamba ni tendo la furaha lakini kwa mwanamke linampa unyonge na wakati mwingine huwa mwanzo wa utumwa wa mapenzi kwa kuogopwa kuachwa wakati tayari ameshatumika!
Hebu jiulize; utatumia/utatumika kwa wangapi? Ukifikiri kwa makini juu ya jibu la swali hili bila shaka utabadilisha mtazamo wako.

(ii) Hupunguza msisimko
Penzi la kienyeji mara nyingi hata wahusika huwa wanajua kabisa kuwa wanakosea. Makosa haya husababisha kupoteza msisimko wa ndani. Ni jambo la kisaikolojia sana na huenda muathirika asigundue tatizo hili kupitia dalili za kitaalamu atakazozionesha.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*