HOT NEWS: ZILIZOBAMBA NCHINI TUNDU LISSU AIMWAGIA SIFA KEDEKEDE SERIKALI YA JPM…

Usiku wa June 29, 2017 zimeripotiwa taarifa mbalimbali kwenye Televisheni za Tanzania ambapo kama ulikosa hii ni time yako kuzisoma hizi kupitia JICHOLETU.COM mbapo miongoni mwa habari nyingi hizi hapa ni kubwa mbili zilizosomwa Channel 10 na TBC1.

Habari ya Channel 10 – Mahakama yawakubali mawakili wapya 248

Mahakama Kuu ya Tanzania imewakubali Mawakili 248 ambao watakwenda kufanya kazi katika Mahakama mbalimbali nchini kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata msaada wa kisheria na kuepuka rushwa.

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma amesema kuongezeka kwa idadi ya Mawakili kutasaidia nchi kufikia malengo yake ikiwemo kutafsiri mikataba mbalimbali na kuwafikishia msaada wa kisheria wananchi walio pembezoni.

>>>“Huo weledi waendele kuwa nao iliwaweze kuwatumikia wananchi, jambo linguine ni swala la madili na rushwa ni swala lisilo la kufumbiwa macho linaongelewa.” Prof. Ibrahim Juma.

“Kwa idadi ya walioingia leo 248, kutakuwa na Mawakili 6,329 ambao ni Mawakili binafsi. Kwa hiyo, kuna uwezokano mkubwa wa kuongezeka kwa huduma za kiwakili na huduma za kisheria kutokana na kuongezeka kwa idadi ya Mawakili. Ni jambo jema” – Tundu Lissu (Rais wa Chama cha Wanasheria).

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*