SAD NEWS: MZEE ALIECHORA NEMBO YA TAIFA AFARIKI DUNIA MUHIMBILI MADAKTARI WAFUNGUKA MAZITO HII LEO…

Francis Maige (Ngosha) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Dar es Salaam. Msanii anayedaiwa kuchora nembo ya Adam na Hawa, iliyotumika kitaifa, Francis Maige (Ngosha) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Ngosha aliyepelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wiki iliyopita kwa ajili ya matibabu, amefariki dunia saa 2 usiku Mei 29.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Hospitali ya Muhimbili imeeleza kuwa hali ya Ngosha ilibadilika ghafla akiwa hospitali hapo.

“Mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha maiti hapa Muhimbili na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa na mamlaka husika.” imesema taarifa hiyo

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*