Asilimia 90 wafanyakazi vyombo vya habari hawana sifa-Utafiti

WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema bado kuna changamoto kubwa katika tasnia ya Habari na Utangazaji baada ya kubainika kuwa asilimia 90 ya wafanyakazi hawana sifa stahiki katika taaluma ya uandishi wa habari na utangazaji

Dk. Mwakyembe amesema katika kusimamia ubora wa huduma za utangazaji, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilifanya ukaguzi kwenye vyombo vya habari na kubaini asilimia 90 ya wafanyakazi hawana sifa stahiki katika taaluma ya uandishi wa Habari na Utangazaji.

“Ili kusimamia ubora wa Huduma za Utangazaji TCRA iliendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye vituo vya utangazaji katika maeneo ya studio, vyumba vya kuandaa habari (Newsroom), maktaba, utaratibu wa ndani wa kuandaa na kutangaza vipindi, sifa za Watangazaji na Waandishi wa Habari na Mikataba ya Ajira, moja ya mambo yaliyobainika katika kaguzi hizo ni asilimia 90 ya wafanyakazi hawana sifa stahiki katika taaluma ya uandishi wa Habari na Utangazaji,” alisema.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*